Sunday, February 6, 2011

Dini na Katiba:

Katiba lazima ibainishe wazi haki na uhuru wa waumini wa dini mbalimbali:
. Je, kila dini inaruhusiwa kuendesha imani zao kwa mujibu wa mafundisho na urithi wao?
. Waislamu wanastahili mahakama ya kdhai?
. Je, kuna chombo chochote cha dini chenye haki ya kuwa na ukiritimba juu ya waumini wa dini au madhehebu fulani? Au kuna uhuru na haki ya kila waumini kuchagua wawe chini ya taasisi gani ya kidini au kimadhehebu?
. Je, dini zina haki ya kuunganisha waumini wa nchi moja na nchi nyingine ili kuwa na mwamvuli mmoja, kwa mfano, Jumuiya ya Wapentakoste au Waislamu wa Afrika Mashariki au Afrika?
. Je, nini haki za dini juu ya wale wanaojenga mabaa na kumbi za starehe au gesti hausi karibu na nyumba zao za ibada ?
. Wanyama ambao ni haramu kwa dini nyingine wanafugwa katika mazingira gani na wale ambao wanyama hao sio haramu?
. Nini haki ya dini moja katika kutumia kitabu au waumini wa dini nyingine kuponda dini fulani?
. Nini haki ya waumini na viongozi wao katika mihadhara na mikutano nje ya nyumba zao za ibada?
. Nini haki ya kila dini kuwa na gazeti, redio na televisheni yake pamoja na biashara zingine? Na serikali isaidieje? Na je televisheni na redio ya taifa itumiwe na dini kwa kiasi gani? Na uwakilishi katika bodi za vyombo hivyo uwe vipi?
. Nini haki ya kila dini kuwa na shule na hospitali na taasisi hizo zipate nini toka serikalini?
. Nani awajibike kuboresha utendaji kazi na menejimenti ya taasisi za kidini?
. Fedha za misaada kwa Waislamu toka nje zirahisishwe vipi kuwafikia na kufanywa yale yanayotakiwa kufanyika bila kuonekana ni fedha za haramu au za kigaidi?
. Je, Siku ya Ijumaa iwe ya Mapumziko kwa Waislamu? Na Jumamosi kwa Wasabato?
Na je, ni haki kuzitumia siku za Ijumaa na Jumamosi kuendesha mikutano wakati ni siku za ibada kwa baadhi ya waumini?
. Je, sherehe za Kiislamu zitambulike kama siku za Mapumziko? Siku gani? Siku ngapi?
. Je, Kalenda ya Kiislamu iambatanishwe katika kalenda za Kirumi au Kizungu?
. Nini kifanyike ili Waislamu waweze kusoma kwa Kiarabu na sio Kiingereza au Kiswahili tu shule za msingi, sekondari na kuendelea ili baadaye iwe rahisi kwao kwenda kujiendeleza katika nchi za Kiarabu?
. Nini kifanyike ili kuona kuwa shule, hospitali na huduma zingine za mashirika ya kidini haziwanyonyi wananchi au kutoa huduma duni kuliko inavyotakiwa na kisha fedha hizo kuliwa na wachache au kwenda kufanya mambo yasiyohusiana na shule husika?