Ibara ya 23 katika kifungu (1) inabainisha kwamba: "Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote,
anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu
wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo
kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya."
Kifungu hiki kinahitaji kupanuliwa ili kutoacha sintofahamu katika masuala muhimu ya ajira, ujira na maslahi ya wafanyakazi.
a) Malipo ya haki ni yepi, yanapimwa vipi, yanarekebishwa vipi na kiwango kinabadilikaje kutokana na mabadiliko katika uchumi na jamii?
b) Kwanini watu wenye ngozi nyeupe, toka nje wanalipwa vizuri kuliko ngozi nyeusi na wazawa kiujumla? Ubaguzi wa aina yoyote hautakiwa kukubalika isipokuwa kama ni ubaguzi wa kumpendelea mzawa.
b) Ni lazima mishahara ioanishwe na kapu la mahitaji ya msingi ya mtu, na kiwango hiki cha chini cha mahitaji ya msingi ndio kiamue ujira wa chini na sio kiwango hiko kuwekwa jinsi wakubwa watakavyo.
c) Mishahara na mapenzi ya rais visiunganishwa. Isiendelee kuonekana kama watu wanapata mishahara kutokana na huruma ya kiongozi huyo.
d) Machelewesho yote ya mfanyakazi au mtumishi wa umma yalipwe riba kwa muda wote utakaocheleweshwa.
e) Makato kwenda NSSF,PPF, LAPF na kwingineko kama huko yawe na kiasi fulani cha ununuzi wa hisa wa mashirika husika. Kinachofanyika hivi sasa ni kuwa wakatwa michango ndio wamiliki wanaostahili, lakini wanaofaidi faida za umilikaji ni serikali na wengineo na sio mwananchi anayestahili kuwa mmilikaji wa mashirika hayo.
f) Mtu yeyote mwenye elimu na ujuzi unaostahili kumfanya aajiriwe lakini hana ajira awe analipwa kiwango na mahitaji ya msingi kwake na familia yake.
g) TUMEWABEBA sana viongozi kwa kuwalipa MISHAHARA MIKUBWA kuliko kazi wanayoifanya katika kuondoa umaskini, ujinga, maradhi na nchi yetu kubaki nyuma kimaendeleo. Kama mwalimu alivyofanya mwaka 1966/7 viongozi wetu walikubali hili; wajione ni wanyonyaji; na mishahara yao iwe nusu kama sio robo ya hii ya leo na iwe inaongezeka kutokana na michango yao katika kuondoa ujinga, umaskini, maradhi katika maeneo yao husika.
h) Wabunge walipwe mishahara inayoendana na elimu, ujuzi na kazi zao za mwisho walizoajiriwa kabla ya kuingia bungeni. Kwa utaratibu huu tutawaondoa wale wote wanaotaka kutajirika kupitia ubunge na siasa.
Wafanyabiashara wote wanaojiingiza katika siasa watatakiwa kujilipa wenyewe bila kugusa senti toka hazina.
i) Ili kujivunia rasilimali watu zetu wenyewe kama Imarati inavyofanya hata pakiwa na bosi toka nje, Mtanzania aliyeko chini yake na anayejifunza kutoka kwake alipwe vizuri kuliko huyo mgeni.
j) Madaktari, manesi, walimu, wahadhiri, wanajeshi na polisi ambao kazi zao haziwaruhusu kufanya (kwa haki) zaidi ya lile waliloajiriwa kama tunataka lifanyike vizuri walipwe mishahara mizuri tu inayowafanya wasitamani kufanya kitu kingine
k) Tofauti kati ya viongozi wa juu na viongozi wa chini na wananchi wengine katika mafao yao baada ya kustaafu yatazamwe na yasipishane kwa kiasi kikubwa na cha kutisha.
l) Wakuu wa mikoa na wilaya kama hawatachaguliwa na wakazi wa mikoa na wilaya husika walipwe na chama tawala.
m) Mishahara miwili iwe marufuku, badala yake mtu apate alawansi inayostahili.
n) Pawe na utaratibu ambao utahakikisha mishahara na mafao ya wafanyakazi ( k.m. EAC) hailiwi na wajanja wachache.
o) Uongezaji mishahara kwa viongozi uendane na jinsi serikali na watumishi wake wanavyochangia kukuza pato la taifa. Likipungua mishahara hiyo ishuke. Likikua mishahara hiyo ipande.
HUU ni mchango wangu katika kusaidia kuwepo kwa katiba bora nchini itakayoweza kutumika sio tu kwa miaka hamsini lakini hata kwa karne kumi na zaidi. Katiba itakayosimama kama katiba na sio matakwa ya mtu fulani au chama fulani hapa nchini.
Saturday, April 30, 2011
Katiba, Dini na Madhehebu
Hadidu za rejea muhimu kwa kipengele hiki kijengwe zaidi kwa ufafanuzi wa ibara ya 19 juu ya Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
i. Nini uwe uhusiano kati ya serikali na dini au madhehebu ?
ii. Nini uwe uhusiano wa wa vyama vya siasa na dini au madhehebu mbalimbali ?
iii. Fidia kwa vyama na na mashirika ya kidini yaliyovunjwa na serikali zilizopita.
iv. Haki ya kila muumini na kila madhehebu kujiunga na kikundi kikubwa au kidogo ili kuendeleza maslahi ya waumini na madhehebu husika na kukataa katakata kikundi chochote kuwa na ukiritimba juu ya waumini wa dini fulani kama ilivyo BAKWATA kwa waislamu.
v. Haki katika kuzipa dini na madehehebu ruzuku.
vi. Uhuru wa kuabudu kwa kuwa na taasisi mbalimbali zinazoendeleza na kulinda imani ya mtu, kwa mfano, Waislamu na Mahakama ya Kadhi.
vii. Taratibu za ugharamiaji taasisi za kidini kutokana na kodi wanayolipwa wanannchi juu ya michango binafasi ya waumini husika.
viii. Haki ya kidemokrasia katika uwakilishi wa taasisi za kidini kutokna na idadi na majukumu ya kila dini, madehehebu na wafuasi wake. Isiwe dini yenye watu wachache ndiyo inayowakilishwa na wawakilishi wengi kuliko ile yenye wafuasi wengi.
ix. Ujenzi wa mahusiano bora na ya amani kati ya dini na dini na madehehebu zao na udhibiti ndani ya dini na miongoni mwa dini kwa wale watakaotaka kutumia dini kuivuruga nchi.
x. Kuoanisha masuala ya kiuchumi na kijamii na maendeleo ya watu ili pasiwe na dini ambayo wafuasi wake wengi ndio matajiri na dini nyingine ambayo waumini wake wengi ndio masikini.

Hoja, Mantiki na sababu za Mkutano wa Katiba Mpya
Katiba mpya ni mkataba sawa na mkataba mwingine wowote. Na kwa sababu hii hapawezi pakawa na pande yoyote katika mkataba inayoweza kuwa muuzaji na mnunuzi kwa wakati huo huo; wakili wa kiapo na shahidi kwa wakati huohuo na mlipaji na mlipwaji kwa wakati huo huo.
Kwa maneno mengine ukiitazama ibara ya 8.-(1) inadhihiisha yafuatayo: " Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata
misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo -
(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa
wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao
kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii.
Ningeliomba tutilie mkazo kwenye vifungu vyenye maneno haya: wananchi ndio msingi wa mamlaka yote; wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao;
Demokrasia na haki ya kijamii;
na lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi.
Kwa uelewa wangu wananchi kuwa msingi wa mamlaka yote ina maana kwamba mabwana na wamiliki wa katiba ni wananchi wenyewe na sio stahili ya mtu yeyote kwa nafasi aliyo nayo kuchukua jukumu hili na kuamua kama vile yeye ndiye wananchi. Haifai. Na sio haki wala halali. Ieleweke na kifungu hiki (wananchi ndio msingi wa mamlaka yote) kama katiba ilivyo sheria mama basi ni kifungu mama cha katiba na hakuna kifungu chochote katika katiba kinaweza kuwa juu yake au kukibatilisha au kukivunja.
Kifungu kinachozungumzia kwamba wananchi watashiriki katika shughuli za Serikali yao ina maana kuna siku au kipindi kitafika na rais, serikali yake, mawaziri, majaji na wabunge watapaswa kukaa pembeni na kuwaachia wananchi wafanye maamuzi yanayowahusu wananchi kama yanavyowahusu viongozi wao. Na kazi kubwa ya serikali inakuwa ni kuwawezesha wananchi kupitia chombo muafaka kitakachowakilisha mawazo, ndoto, kero, kutoridhika, maudhi, dhamira, matamanio na maslahi yao kwa mapana na marefu kuifanya kazi iliyoko mbele ya taifa. Ieleweke kuwa ushiriki huu wa wananchi katika serikali yao hufanyika mara chache katika maisha ya taifa husika.
Lakini ni ushiriki muhimu mno kiasi kwamba huaminika kwamba muda kama huu ndio unaobainisha kati ya viongozi bora na viongozi duni na wapowapo tu, katika historia ya nchi husika.
Ninachukulia pia kwamba kifungu kinachozungumzia Demokrasia na haki ya kijamii kina maana katika wakati kama huo haki inakuwa ni kile kitendo cha kiongozi wa nchi aliyepo kukubali kwamba wanaostahili kufanya maamuzi husika ni wananchi na siyo yeye na neno demokrasia linaimanisha kwamba walio wengi ndio watakaoamua. Au pale inapolazimika wasio na ubinafsi na wanaoona mbali zaidi ya wananchi wengine ndio waamue.
Ninachukulia pia kwamba katika mchakato kama huu uliopo mbele yetu maneno: " lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi," yaana maana kwamba katika kipindi kama hiki serikali inastahili kuwa inatafakari jinsi gani lengo hili la ustawi litaoanishwa na katiba mpya kwa namna ambayo vyote, yaani, serikali na katiba wakati utakapofika vitaonekana kufanya kazi kwa ufanifu na ufanisi uliokusudiwa.
Na hasa ukizingatia pamoja na kwamba tulipata uhuru sawa na Malaysia, Botswana, Singapore, Indonesia, nchi mbalimbali za Kiarabu hivi leo, miaka 50 baada ya uhuru, hatuzioni hata indiketa za magari yao ya kimaendeleo ziko wapi.
Ukifika wakati kama huu kiongozi wa nchi anapaswa awe juu ya siasa, vyama na serikali yenyewe na akajiwezesha na kuwezeshwa kuyaweka mbele maslahi ya nchi na watu wake na kutambua kwamba kazi iliyoko mbele yake ni kazi itakayomjengea jina, heshima na shukrani zisizokwishamilele kama baba wa demokrasia na utaifa katika nchi husika. Ni nafasi kama hii tu inayozaa viongozi ambao maamuzi yao yanaitoa nchi na fikra za wananchi wake kutoka kwenye kizazi ambacho mambo yake yamepitwa na wakati kuingia kwenye kujali na kuzingatia maslahi na manufaa ya walio wengi kwa kizazi kilichopo na vile vitakavyokuja baada ya hapa. Huu ni wakati wa pekee unaotoa rais ambaye maamuzi yake yanakuwa ni makubwa kuliko maslahi binafsi ba maslahi ya chama chake. Huu ni wakati unaotoa rais ambaye kweli ni rais wa wote na sio wale tu wa chama chake na waliompigia kura. Huu ni wakati wa kuiunganisha nchi ambayo tayari ilikuwa ikitishiwa na kusambaratika kutokana na sababu mbalimbali.
Uamuzi katika hatua kama hii ndio unaoamua kama vyama vya siasa vitakuwa ni chombo imara na bora na vinavyotegemewa na wananchi au la; umaskini utapunguzwa au utaongezeka; ufisadi utakwisha au utakuwa kama funza na kujichimbia chini kwa chini; rasilmali watu bora itaongezeka na wote kupatiwa kazi au tatizo la wajuzi na ajira litaendelea kuiandama nchi na vijana wake na maji yanayotuzunguka yatatiririshwa na kutufikia majumbani au yataendelea kuishia maporini na kunyonywa na jua.
Uamuzi huo pia unaoamua tutakuwa na bunge la watu waliobalehe kimwili, kitabia, kimaamuzi na kifikra, kama tutakuwa na dini zinazoheshimiana au zisizoheshimiana; amani na umoja au kinyume cha hivyo; kila Mtanzania kuwa na nyumba kama hitaji la msingi au nyumba kuwa kwa wale waliochaguliwa au kupendelewa tu; umeme utakuwepo katika kila nyumba au ni asilimia 5 ya Watanzania watakaokuwa na umeme.
Baada ya kuizungumzia ibara ya 8 hebu tuangalie yaliyomo katika ibara ya 9 na kujiuliza kama kweli kuna chombo chochote zaidi ya baraza au mkutano wa katiba mpya unaoweza kukidhi malengo ambayo yamo katika katiba iliyopo hivi sasa kwa mapana na marefu yake na kisiwe kinarashiarashia tu na kushindwa kutimiza maazimio hayo na matarajio ya Watanzania wa leo na kesho:
Katika ibara hii kwa maoni yangu ninaamini ndio kuna kiini maridhawa cha uandikaji wa katiba mpya. Kwanza, ipo fursa ya kukubali au kukataa kama nchi hii ni ya kijamaa au la. Na kwa sababu wote tulihusishwa katika suala la ujamaa na kujitegemea tutawatendea haki wananchi wetu pale tutakapowapa fursa ya wao wenyewe kujadili kwa mapana na marefu juu ya kukubali au kuukataa ujamaa. Na kisha wafanye maamuzi juu ya mfumo mpya wa kisiasa wanaoamini utawaharakishia maendeleo yao na utakaoweza kuwafaa kwa miaka 50-100 ijayo.
Baada ya hapo unafuata msururu wa mambo ambayo Watanzania inasemekena kwa niaba ya chama tawala/chama kimoja waliamua kuwa ndiyo mkataba wa malengo na majukumu wanayostahili kubeba watawala ili watawaliwa waridhike na waone wanatendewa ipasavyo:
NInaiorodhesha hapa chini na pembeni yake kukiwa na swali la msingi, yaani, je bila kuwa na baraza au mkutano wa katiba mpya tutaweza kweli kutenda haki kwa Watanzania wa leo na vizazi vyao vijavyo ?
Kifungu (a) kinasema kwamba ni kazi ya watawala kuhakikisha: " kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu
zinaheshimiwa na kuthaminiwa," je tathmini ya hili linaweza kweli kufanyika na kundi la watu wachache tu katika jamii ambao hawaijui hata 1/100 ya nchi au ni baraza au mkutano wa katiba ambao pengine una wabunge wote; wawakilishi kutoka kila wilaya nchini; wawakilishi wanaowakilisha maslahi ya kila kundi nchini wakiwemo wafanyakazi, wakulima, wafugaji, wavuvi, wawindaji, wanafunzi, vijana, wazee, wanawake na kadhalika?
Kifungu (b) kinataka serikali kuhakikisha : "kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa," ni nani anayeweza mchakato wa kuonesha hili linafanyika au halifanyiki ipasavyo na ni kwa sababu gani na nini kifanyike ili lifanyike ipasavyo?
Kifungu kingine muhimu ni kile cha (c) ambacho kinaiamuru serikali kuhakikisha : " kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia
ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa
unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa
manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia
mtu kumyonya mtu mwingine," na baada ya mali za umma kubinfasishwa na wananchi wasirudishiwe kodi/michango yao, CCM kuchukua mali zilizojengwa na jasho na fedha yawananchi, migodi kukodishwa kwa mrabaha sawa na hamna kitu na mikakati ya kupunguza umaskini kukwama, je tunastahili kuwa na chombo cha namna gani kuandika katiba kama sio baraza au mkutano wa katiba mpya?
Nchi iliyobarikiwa kuwa na Azimio la Arusha na maamuzi ya busara kama vile kuziweka njia zote kuu za uchumi chini ya umma ni kichekesho leo kugawa migodi ya madini ovyo kama njugu kwa watu wasio na mapenzi na uchungu na watu wetu na maendeleo yao. Nchi ambayo inajua unyama na unyonyaji wa mabenki inasikitisha kuona kwamba imebinafsisha mabenki ambayo lengo lake ni kuwakaanga Watanzania katika mafuta yao wenyewe. Nchi ambayo inajua faida za ujamaa na kujitegemea inaaibisha kuiona leo inakaribisha wawekezaji kama wale wa simu za mkononi ambao lengo lao ni kupanda na kuvuna papo kwa hapo huku wakifaidika vilivyo na misamaha ya kodi.
Hoja yetu inabakia pale pale kwa vifungu vilivyobakia vifuatavyo: " (d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake; (f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na
kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la
Dunia kuhusu Haki za Binadamu; (g) kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa
waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya
mtu; (h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi,
rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini; (i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha
umaskini, ujinga na maradhi;
(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia
kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi; na
(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya
demokrasia."
Kwa kuwa wananchi ndio msingi wa mamlaka yote wana haki ya kurejesha mamlaka yao kwa muda na wakawapangia watumishi wao majukumu upya. Uundwaji wa katiba mpya unahitaji marejesho haya ya mamlaka kwa muda kwa wananchi. Ni kitendo cha heshima, utii, uaminifu na kiungwana kwa wapiga kura kufanya hivyo katika wakati kama huu.
Ni muhimu kwa wanasiasa na vyama siasa kuwa na imani na wananchi wakati huu. Na ni chama na wanasiasa watakaokuwa na imani na wananchi, na wananchi wakawa na imani nao ndio watakaokuwa cha ushindi kwa wananchi wote.
Ushauri bora wa hivi karibuni ni ule uliotolewa wakati wa pasaka ukisema ya kwamba:' kuandika katiba mpya si sawa na kuandika ilani ya chama fulani cha kisiasa.'
Aidha, vyama vya upinzani havina haki ya kutaka kuandika katiba kwa madhumuni ya kukiondoa chama tawala madarakani, kama ilivyo kwa chama tawala kutotamani kuandika katiba ili kuvizuia vyama mbadala kuja kuingia madarakani wakati ufikapo.
Tujiulize kwa hiyo je, ni baraza ama mkutano wa katiba mpya ambacho kitakuwa chombo kinachoundwa na wananchi wenyewe kupitia wawakilishi wao au Tume ya hiki au kile itakayoundwa kwa kupora mamlaka na madaraka ya wananchi ndicho kitakachoweza kuyashughulikia masuala haya kwa ukamilifu na haki zaidi? Budi fikra za viongozi wetu ziwe kubwa kuliko za kiserikali, kiungozi, kisiasa, kivyama na kibinafsi katika kufanya uamuzi sahihi na muafaka kuhusu kazi iliyoko mbele yetu.

Subscribe to:
Posts (Atom)