Ibara ya 23 katika kifungu (1) inabainisha kwamba: "Kila mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote,
anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu
wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo
kulingana na kiasi na sifa za kazi wanayoifanya."
Kifungu hiki kinahitaji kupanuliwa ili kutoacha sintofahamu katika masuala muhimu ya ajira, ujira na maslahi ya wafanyakazi.
a) Malipo ya haki ni yepi, yanapimwa vipi, yanarekebishwa vipi na kiwango kinabadilikaje kutokana na mabadiliko katika uchumi na jamii?
b) Kwanini watu wenye ngozi nyeupe, toka nje wanalipwa vizuri kuliko ngozi nyeusi na wazawa kiujumla? Ubaguzi wa aina yoyote hautakiwa kukubalika isipokuwa kama ni ubaguzi wa kumpendelea mzawa.
b) Ni lazima mishahara ioanishwe na kapu la mahitaji ya msingi ya mtu, na kiwango hiki cha chini cha mahitaji ya msingi ndio kiamue ujira wa chini na sio kiwango hiko kuwekwa jinsi wakubwa watakavyo.
c) Mishahara na mapenzi ya rais visiunganishwa. Isiendelee kuonekana kama watu wanapata mishahara kutokana na huruma ya kiongozi huyo.
d) Machelewesho yote ya mfanyakazi au mtumishi wa umma yalipwe riba kwa muda wote utakaocheleweshwa.
e) Makato kwenda NSSF,PPF, LAPF na kwingineko kama huko yawe na kiasi fulani cha ununuzi wa hisa wa mashirika husika. Kinachofanyika hivi sasa ni kuwa wakatwa michango ndio wamiliki wanaostahili, lakini wanaofaidi faida za umilikaji ni serikali na wengineo na sio mwananchi anayestahili kuwa mmilikaji wa mashirika hayo.
f) Mtu yeyote mwenye elimu na ujuzi unaostahili kumfanya aajiriwe lakini hana ajira awe analipwa kiwango na mahitaji ya msingi kwake na familia yake.
g) TUMEWABEBA sana viongozi kwa kuwalipa MISHAHARA MIKUBWA kuliko kazi wanayoifanya katika kuondoa umaskini, ujinga, maradhi na nchi yetu kubaki nyuma kimaendeleo. Kama mwalimu alivyofanya mwaka 1966/7 viongozi wetu walikubali hili; wajione ni wanyonyaji; na mishahara yao iwe nusu kama sio robo ya hii ya leo na iwe inaongezeka kutokana na michango yao katika kuondoa ujinga, umaskini, maradhi katika maeneo yao husika.
h) Wabunge walipwe mishahara inayoendana na elimu, ujuzi na kazi zao za mwisho walizoajiriwa kabla ya kuingia bungeni. Kwa utaratibu huu tutawaondoa wale wote wanaotaka kutajirika kupitia ubunge na siasa.
Wafanyabiashara wote wanaojiingiza katika siasa watatakiwa kujilipa wenyewe bila kugusa senti toka hazina.
i) Ili kujivunia rasilimali watu zetu wenyewe kama Imarati inavyofanya hata pakiwa na bosi toka nje, Mtanzania aliyeko chini yake na anayejifunza kutoka kwake alipwe vizuri kuliko huyo mgeni.
j) Madaktari, manesi, walimu, wahadhiri, wanajeshi na polisi ambao kazi zao haziwaruhusu kufanya (kwa haki) zaidi ya lile waliloajiriwa kama tunataka lifanyike vizuri walipwe mishahara mizuri tu inayowafanya wasitamani kufanya kitu kingine
k) Tofauti kati ya viongozi wa juu na viongozi wa chini na wananchi wengine katika mafao yao baada ya kustaafu yatazamwe na yasipishane kwa kiasi kikubwa na cha kutisha.
l) Wakuu wa mikoa na wilaya kama hawatachaguliwa na wakazi wa mikoa na wilaya husika walipwe na chama tawala.
m) Mishahara miwili iwe marufuku, badala yake mtu apate alawansi inayostahili.
n) Pawe na utaratibu ambao utahakikisha mishahara na mafao ya wafanyakazi ( k.m. EAC) hailiwi na wajanja wachache.
o) Uongezaji mishahara kwa viongozi uendane na jinsi serikali na watumishi wake wanavyochangia kukuza pato la taifa. Likipungua mishahara hiyo ishuke. Likikua mishahara hiyo ipande.
No comments:
Post a Comment