Hadidu za rejea muhimu kwa kipengele hiki kijengwe zaidi kwa ufafanuzi wa ibara ya 19 juu ya Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
i. Nini uwe uhusiano kati ya serikali na dini au madhehebu ?
ii. Nini uwe uhusiano wa wa vyama vya siasa na dini au madhehebu mbalimbali ?
iii. Fidia kwa vyama na na mashirika ya kidini yaliyovunjwa na serikali zilizopita.
iv. Haki ya kila muumini na kila madhehebu kujiunga na kikundi kikubwa au kidogo ili kuendeleza maslahi ya waumini na madhehebu husika na kukataa katakata kikundi chochote kuwa na ukiritimba juu ya waumini wa dini fulani kama ilivyo BAKWATA kwa waislamu.
v. Haki katika kuzipa dini na madehehebu ruzuku.
vi. Uhuru wa kuabudu kwa kuwa na taasisi mbalimbali zinazoendeleza na kulinda imani ya mtu, kwa mfano, Waislamu na Mahakama ya Kadhi.
vii. Taratibu za ugharamiaji taasisi za kidini kutokana na kodi wanayolipwa wanannchi juu ya michango binafasi ya waumini husika.
viii. Haki ya kidemokrasia katika uwakilishi wa taasisi za kidini kutokna na idadi na majukumu ya kila dini, madehehebu na wafuasi wake. Isiwe dini yenye watu wachache ndiyo inayowakilishwa na wawakilishi wengi kuliko ile yenye wafuasi wengi.
ix. Ujenzi wa mahusiano bora na ya amani kati ya dini na dini na madehehebu zao na udhibiti ndani ya dini na miongoni mwa dini kwa wale watakaotaka kutumia dini kuivuruga nchi.
x. Kuoanisha masuala ya kiuchumi na kijamii na maendeleo ya watu ili pasiwe na dini ambayo wafuasi wake wengi ndio matajiri na dini nyingine ambayo waumini wake wengi ndio masikini.
No comments:
Post a Comment