Monday, January 31, 2011

Makazi ya Watu, Mabaa na Ustaarabu

KUMEZUKA mtindo wa viongozi na watendaji katika ngazi za chini kudharau imani misimamo ya wakazi mitaani kitu ambacho kinaashiria kuhatarisha umoja na amani nchini.

Baa, vilabu na maeneo mengine ya starehe kwa upande wa Waislamu, Walokole na watu wa dini nyingine wanaopenda kulea watoto wao katika maadili yanayokubalika visijengwe hadi wakazi wote wameridhia.

Serikali za mitaa hazina sauti kuliko wakazi wa mitaa husika. Na uroho na ulafi wa viongozi usiwe chimbuko la kuwageuza wananchi kuwa wavunja sheria na katiba wakati ni viongozi na mabwana zao ndio wanaovunja katiba.

Kwa mfano hili la ujenzi wa baa na vilabu vya starehe na ngono ovyo ovyo kila mahala kiasi kwamba sasa inakuwa ni vigumu kwa wakazi mitaani kulala na kupumzika kwa amani. Juu ya hili unaongezewa magari yanayopita mitaani na makelele na promosheni za kijinga na zisizoendana na maadili ya Watanzania.

Ni lazima katiba imlinde mwananchi wa kawaida na sio matajiri na wenye fedha na viongozi na hasa wale wenye mabaa na vilabu vya starehe!

Hadidu:
. Baa zijengwe karibu na misikiti, kanisa na makazi ya watu?
. Maduka ya Pombe na Baa ziwepo kwenye maeneo ya watu wenye imani zinazokataza vitu hivyo?
. Kuwe na utaratibu gani wa kuzuia polusheni ya sauti na makelele watu wasiyotaka kusikia?
. Ni nani aruhusu ujenzi wa baa karibu na makazi ya wananchi? Wananchi wenyewe au maofisa serikali na viongozi wa vyama waroho na walafi?
. Malaya waendeshe biashara zao kwa utaratibu gani na mahala gani?
. Wasenge na mabaasha wawe na haki gani katika jamii ya Kitanzania?
. Baa ziruhusiwe kuwa kwenye maeneo ya wazi na kuwatamanisha watoto na vijana wa waumini ambao kwao ni haramu?

No comments:

Post a Comment