ILI kufanikisha uandikwaji katiba mpya ninapendekeza yafuatayo, bila ushawishi kutoka kwea yeyote:
1. Mheshimiwa rais asitishe kuchagua tume yake ya katiba;
2. Muswaada wa uundwaji wa tume ya katiba urejeshwe bungeni baada ya kufanyiwa kazi na wataalam wa Katiba kama Maprofesa Issa Shivji na Chris-Peter Maina.
3. Taifa liunde Baraza la Kikatiba litakalotokana na wawakilishi wa makundi maslahi mbalimbali, vyama vya kisiasa, taasisi za kidini, wabunge na kadhalika:
4. Tume ya Uchaguzi inayonukia Uchama iliyopo ivunjwe. Tume Huru ya Uchaguzi ichaguliwa na Baraza Jipya la Kikatiba, kama uthibitisho kwamba mamlaka sasa imerudishwa mikononi mwa wananchi;
5. Baraza Jipya la Kikatiba likishirikiana na ofisi ya rais kuteua Waziri mpya wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
6. Baraza Jipya la Kikatiba liteue Kamati Maalum Kushughulikia upatikanaji maoni na uandikwaji wa Katiba mpya;
7. Maamuzi yote yanayopitukia Chama Kimoja na masuala ya demokrasia yaamuliwe na Baraza Jipya la Kikatiba badala ya Serikali au Ikulu ili kulinda amani na umoja wa nchi;
8. Mapendekezo ya Kikatiba yagawanywe kait ya yale yanayostahili kushughulikiwa moja kwa moja na kwa haraka sana na yale yanayoweza kutekelezwa baada ya Katiba mpya kupitishwa;
9. Ili kuiepusha nchi na gharama zisizo za lazima wakati huu mgumu kiuchumi, Mahakama na Mwanasheria Mkuu wa serikali badala ya kuingilia uhuru wa vyama vya upinzani wapitishe sheria ya kuruhusu mgombea huru wa uchaguzi, na kwa maana hiyo, ruhusa ya mbunge anayefukuzwa toka chama fulani kuendelea na ubunge wake kama mbunge asiye na chama au mbunge huru;
10. Baraza jipya la Katiba kuruhusu vyama, mashirika yasiyo ya kiserikali, wanaharakati, wanasheria na vyama vya kijamii mbalimbali kutumia kipindi cha mwaka huu kuwaelimisha Watanzania juu ya katiba ya zamani na mbinu na mikakati ya kuwa na katiba itakaowafaa Watanzania kwa miaka 50 au zaidi.
11. Baraza jipya la katiba litaunda kamati au vyombo maalum vya kitaalaamu ambavyo kwa ushirikiano na makundi maslahi katika jamii yetu vitafanya mchakato wa kuhakikisha kila kisichopo katika katiba kinazungumzwa na kisha kuingizwa katika katiba kwa mujibu ya matakwa ya watawaliwa wa nchi hii.
12. Baraza jipya la katiba litaunda kamati na vyombo mbalimbali vya kitaalamu kupitia ibara na vifungu vyote ambavyo vimekoslewa kwa njia moja au nyingine ili kuviboresha au kuviondoa kabisa kama havifai.
Mawazo mazuri sana brother
ReplyDeleteMawazo mazuri sana brother
ReplyDelete